Match Day : Yanga vs Ihefu Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jul 2021
Match Day : Yanga vs Ihefu Fc

Alhamisi ya leo Julai 15 2021, kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ihefu Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Huu ni mchezo maalum kwa Yanga na kiungo Haruna Niyonzima ambaye mchezo huo utatumika kumuaga rasmi baada ya kuitumikia Yanga kwa takribani misimu sita

Aidha siku ya leo kabla ya mchezo, Azam Media na Yanga watakuwa na jambo lao pale uwanja wa Benjamin Mkapa

Tukirudi kwenye mchezo wenyewe, Yanga inahitaji angalau alama moja tu ili kujihakikishia wanamaliza katika nafasi mbili za juu na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi mabingwa msimu ujao

Hata hivyo hautakuwa mchezo mwepesi, kwani Ihefu Fc nao wanazihitaji alama zote tatu ili kujinusuru na hatari ya kuteremka daraja

Katika mchezo wa leo huenda baadhi ya wachezaji waliokosekana kikosini kwa wiki kadhaa wakarejea

Nahodha Lamine Moro na Michael Sarpong walirejeshwa kikosini baada ya kumaliza changamoto na uongozi

Jana katika mkutano na Wanahabari, Mkufunzi wa makipa Razak Siwa alisema kwao bado ligi haijamalizika wanahitaji kuzipata alama zote sita kutoka katika michezo miwili iliyobaki wakianza leo dhidi ya Ihefu Fc

Ni saa kumi kamili jioni pale uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
56m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’