Yanga ya Nabi ni raha tupu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2021
Yanga ya Nabi ni raha tupu

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi kwa sasa ni mtu mwenye raha sana baada ya kazi yake kuanza kuonyesha matunda

Ndio! matunda yanaonekana kwani kwa sasa Yanga sio ile ambayo mashabiki walilazimika kushika mioyo yao kwa dakika zote tisini

Yanga ya Nabi sio ile butua butua aliyoiasisi Zlatko Krmpotic na sio ile ya Cedric Kaze ambayo ilikuwa ikikata 'moto' katika kipindi cha pili!

Yanga ya Nabi sio ile iliyokuwa ikitengeneza nafasi mbili ndani ya dakika 90, sasa nafasi za kufunga mabao zinatengenezwa kwa wingi

Yanga ya Nabi ina Feisal Salum 'fei Toto' aliyezaliwa upya ukilinganisha na yule Fei Toto aliyekuwa kipindi cha nyuma

Chini ya Nabi, Fei Toto ndiye nyota wa kikosi cha Yanga akiweka kambani mabao manne na kutoa pasi kadhaa za mabao

Wakati huu ni raha kuwa shabiki wa Yanga, kama uko uwanjani unakaa kwa kujiamini jukwaani kwani una uhakika utashangilia mabao

Kwa wale wanaoshuhudia mechi kupitia Azam Tv iwe nyumbani au 'vibanda umiza', utawakuta mapemaa wanasubiria 'mbungi' wakiwa na tabasamu nyusoni mwao

Hapa tunaizungumzia Yanga ya kocha Nasreddine Nabi ambayo imeshinda michezo saba mfululizo!

Huyu mwamba amepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Azam Fc, tena ulikuwa mchezo wake wa kwanza kabisa akiwa bado hajaingiza mbinu zake kwenye timu

Msimu unamalizika, Wananchi watarajie mambo mazuri zaidi msimu ujao kwani kama wachezaji hawa aliowakuta kawaboresha hivi je akiongeza na wake wapya itakuwaje?

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’