Ligi inafika tamati leo, Yanga wako Dodoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jul 2021
Ligi inafika tamati leo, Yanga wako Dodoma

Hatimaye ligi kuu ya Vodacom inafikia tamati leo kwa timu zote 18 kushuka viwanjani

Wakati nafasi nne za juu zikiwa tayari zimethibitishwa, vita kubwa iko chini ya msimamo ambao timu nyingine tatu za kushuka daraja zitafahamika leo kuungana na Mwadui Fc

Aidha timu nyingine mbiliΒ  zitazoshika nafasi ya 14 na 13 zitacheza play-off na timu nyingine mbili kutoka ligi daraja la kwanza kuwania nafasi ya kupanda/kubaki au kushuka kwa timu za VPL

Wananchi wao wako mkoani Dodoma kumenyana na Dodoma Jiji katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Jamhuri

Yanga itashuka dimbani ikiwa haina presha yoyote ya matokeo katika mchezo huo kwani tayari imejihakikishia kumaliza kwenye nafasi ya pili

Pengine kocha Nasreddine Nabi atawapa mapumziko baadhi ya wachezaji wake muhimu kwani ikumbukwe wiki ijayo Wananchi wana mchezo muhimu wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya watani zao Simba

Mchezo huo utapigwa Jumapili ijayo katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma

Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’