Hatimaye ligi kuu ya Vodacom inafikia tamati leo kwa timu zote 18 kushuka viwanjani
Wakati nafasi nne za juu zikiwa tayari zimethibitishwa, vita kubwa iko chini ya msimamo ambao timu nyingine tatu za kushuka daraja zitafahamika leo kuungana na Mwadui Fc
Aidha timu nyingine mbiliΒ zitazoshika nafasi ya 14 na 13 zitacheza play-off na timu nyingine mbili kutoka ligi daraja la kwanza kuwania nafasi ya kupanda/kubaki au kushuka kwa timu za VPL
Wananchi wao wako mkoani Dodoma kumenyana na Dodoma Jiji katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Jamhuri
Yanga itashuka dimbani ikiwa haina presha yoyote ya matokeo katika mchezo huo kwani tayari imejihakikishia kumaliza kwenye nafasi ya pili
Pengine kocha Nasreddine Nabi atawapa mapumziko baadhi ya wachezaji wake muhimu kwani ikumbukwe wiki ijayo Wananchi wana mchezo muhimu wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya watani zao Simba
Mchezo huo utapigwa Jumapili ijayo katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni
Β