Kalenda ya Michuano ya CAF imetolewa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2021
Kalenda ya Michuano ya CAF imetolewa

Jana Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) liliweka hadharani kalenda ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho kwa msimu ujao 2021/22

Kalenda hiyo inaonyesha kuwa michezo ya hatua ya awali itapigwa mwezi Septemba ambapo mchezo wa kwanza utapigwa kati ya tarehe 10-12 Septemba na marudiano kupigwa kati ya tarehe 17-19 Septemba 2021

Hii ina maana baada ya mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambao utapigwa Jumapili ijao, Julai 25 mkoani Kigoma, kutakuwa na takribani mwezi mmoja na wiki mbili za kujiandaa na michuano hiyo kwa timu za Tanzania ambazo ni Simba, Yanga, Azam Fc na Biashara United

Ni wazi hakutakuwa na muda mrefu wa mapumziko kwa wachezaji kutokana na ligi yetu kuchelewa kumalizika, vinginevyo hakutakuwa na muda wa kutosha kujiandaa

Hapa pia linakuja suala la usajili ambapo dirisha lilifunguliwa jana na litafungwa August 31, 2021. Kamati inayosimamia usajili wanapaswa kuhakikisha wanakamilisha mapema michakato yote ya usajili ili wachezaji wote waanze pamoja maandalizi

Msimu uliomaliza, Yanga iliuanza kwa kusuasua kutokana na changamoto ya kuchelewa kocha na baadhi ya wachezaji

Ukiangalia kama mchezaji atasajiliwa August 31, atakuwa na wiki mbili za kufanya mazoezi na wenzake muda ambao hauwezi kutosha kwake kuingia katika kikosi

Inapaswa mpaka kufikia mwisho wa mwezi huu, kuwa michakato yote ya usajili ikamilike ili maandalizi yatakapoanza mwanzoni mwa August wachezaji wote wapo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’