Sare zilituvurugia hesabu - Bumbuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jul 2021
Sare zilituvurugia hesabu - Bumbuli

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wamedhamiria kumaliza msimu kibabe kwa kuibuka na ubingwa wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kuwafunga watani zao Simba baada ya kukosa ubingwa wa ligi kuu

Kikosi cha Yanga kilirejea jijini Dar es salaam jana wakitokea Dodoma ambako walikamilisha msimu wa ligi kuu kwa kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Dodoma Jiji

Bumbuli amesema malengo waliyokuwa nayo wakati msimu unaanza ilikuwa kushinda kila taji waliloshiriki ikiwemo ubingwa wa ligi kuu

Hata hivyo wameshindwa kutwaa taji la VPL baada ya kupata sare nyingi katika mechi ambazo walipaswa kushinda

"Timu imerejea Dar es salaam na moja kwa moja kuingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wetu wa fainali dhidi ya Simba, huo ndiyo utakuwa mchezo wetu wa mwisho msimu huu na tumedhamiria kushinda ili kuwa mabingwa wa kombe la FA" alisema Bumbuli.

"Tumekosa ubingwa wa ligi kuu kutokana na makosa ambayo tuliyafanya, tulipata sare nyingi lakini yote kwa yote, sisi tumeyaacha, tunasonga mbele. Kama kauli mbiu yetu inavyosema, Yanga daima mbele nyuma mwiko, kwa hiyo tunaangalia yajayo wala si yaliyopita"

Yanga ndio timu pekee iliyofungwa michezo michache msimu uliomalizika, wakipoteza michezo miwili tu dhidi ya Coastal Union na Azam FC

Hata hivyo michezo waliyotoka sare ni 11, ambayo ndiyo iliyovuruga hesabu za ubingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
53m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’