Kuelekea mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho katika uwanja wa Lake Tanganyika, Serikali mkoani Kigoma imewaasa mashabiki kuvaa barakoa na kunawa mikono siku ya mtanange huo
Akizungumza na Wanahabari jana, Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye alisema tahadhari hiyo sio tu watakaoingia uwanjani hata wataokuwa wanaangalia mpira kwenye televisheni mitaani nao wavae barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka
"Serikali ya mkoa inaeleza yafuatayo, watu wote wataoingia uwanjani kuangalia mpira wahakikishe wamevaa barakoa muda wote wa mchezo”
“Serikali imehakikisha uwepo wa maji, watu wanawe mikono kabla ya kuingia uwanjani,"alisema Andengenye
Mchezo huo wa watani wa jadi, utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni ambapo mshindi ataondoka na kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)