Yanga iko mbioni kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Francis Kazadi Kasengu raia wa DR Congo, imefahamika
Kazadi anatarajiwa kutua Jangwani kwa mkopo akitokea klabu ya Wydad Athletic,mabingwa Morocco
Msimu uliopita, Kazadi ambaye pia anaweza kucheza kama winga, aliitumikia Al Masry ya nchini Misri kwa mkopo
Kabla ya kutimkia Wydad Athletic, Kazadi aliitumikia klabu ya AS Vita akikumbukwa kupachika bao katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Simba uliopigwa jijini Dar es salaam msimu wa 2018/19
Yanga sasa inaweza kuwa imekamilisha usajili wa wachezaji watatu kutoka DR Congo ambao ni Shabani Djuma, Fiston Mayele na Kazadi ambapo wote wako katika timu ya Taifa
Hawa watakutana na kina Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda huku pia Wananchi wakihusishwa na kumrejesha mshambuliaji Heritier Makambo ambaye hivi karibuni alivunja mkataba wake na Horoya Ac
Baada ya mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba hapo kesho, Wananchi wataanza kuweka hadharani nyota wapya
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindao Injinia Hersi Said alidokeza kuwa usajili umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90