Haikuwa siku nzuri sana kwa kiungo Mukoko Tonombe ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika za majeruhi kipindi cha kwanza baada ya kumpiga kiwiko John Bocco
Ni presha ya mchezo iliyomkumba Mukoko baada ya kufanyiwa madhambi na Bocco
Ikumbukwe katika mchezo wa Julai 03 uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Mukoko alifanyiwa rafu nyingi na Bocco pasipo mwamuzi kuchukua hatua yoyote
Pengine leo hakuweza kuwa mvumilivu na kujikuta akifanya kosa ambalo kwa hakika limeigharimu Yanga
Wakati mwingine matukio haya hutokea pasipo kutarajiwa, ni kosa ambalo Mukoko atalijutia kwa muda mrefu
Jambo muhimu kwa Wanayanga ni kumjenga kisaikolojia kwa kutompa presha kutokana na tukio lile
Dabi nyingine inakuja mwezi Septemba Ngao ya Jamii, hawa bado tunao...!
ADVERTISE HERE