Tuko katika njia nzuri ya mafanikio - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jul 2021
Tuko katika njia nzuri ya mafanikio - Injinia Hersi

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga Injinia Hersi Said amewataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga wasiwe wanyonge kwani wako katika njia nzuri ya mafanikio

Hersi amesema wao kama viongozi wameridhishwa na kuimarika kwa timu msimu huu na hakubaliani na mtu yeyote anayesema Yanga ina kikosi dhaifu

Aidha Hersi amesisitiza kuwa kujenga timu imara sio jambo la siku moja, lakini walichokiona mpaka sasa kimewapa matumaini kuwa wako katika njia sahihi

"Ukisema hatuna kikosi kipana siwezi kukuelewa, tumekuwa na timu nzuri msimu huu. Vijana wamepambana vyema na sisi kama viongozi, wanachama na wapenzi wa timu hii tunajivunia jitihada zao"

"Tutafanya usajili mzuri kwa maelekezo ya kocha ili kuendelea kuisuka vyema timu yetu. Msimu huu tulikuwa WASHINDANI ila msimu ujao tutakuwa WASHINDI," alisema Hersi

"Tumeshika nafasi ya pili ligi kuu Tanzania bara, fainali ASFC na ubingwa Mapinduzi Cup. Itoshe kusema tulikuwa katika build up nzuri kuanzia wachezaji na benchi la ufundi"

"Soka lina njia zake katika kulijenga kwa maana ya kutengeneza timu ya ushindi na klabu ya mafanikio. Nina imani kwa kudra za mwenyezi Mungu , ushirikiano wetu sote; viongozi na wanachama, msimu ujao tutakuwa na timu nzuri ya USHINDI na maendeleo ya klabu yetu kwa michakato ya mabadiliko inayoendelea"

"Wapenzi, mashabiki na wanachama wetu wasiwe wanyonge bali wajione wapo katika njia nzuri ya mafanikio ambayo inajengwa vyema ili kuleta matunda mazuri kwa muda mrefu ujao"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’