Mchezo wa ufunguzi wa michuano ya kombe la Kagame uliozikutanisha Yanga na Nyasa Big Bullets umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1
Yanga ilitangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa Waziri Junior aliyeunganisha vyema krosi ya Dickson Ambundo aliyekuwa akiisumbua safu ya ulinzi ya Big Bullets
Big Bullets wakasawazisha kupitia mkwaju wa penati baada ya nahodha Abdallah Shaibu Ninja kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Nyasa Big Bullets ndani ya eneo la hatari
Yanga ilikabiliwa na changamoto ya kukosa muungano kwani ukiondoa Waziri Jr, wachezaji wengine walianza katika safu ya kiungo na ushambuliaji walikuwa wageni
Mashabiki wa Yanga wamepata nafasi ya kuwaona nyota wawili wapya Dickson Ambundo na Jimmy Ukonde wachezaji hao wakishuka dimbani bila ya kuwa na mda wa kufanya mazoezi na wenzao
Ukonde na Ambundo waliingia kambini usiku wa kuamkia leo, lakini kila mmoja ameonyesha ubora alionao



