Baada ya kukamilika michuano ya kombe la Kagame, kikosi cha Yanga kitaelekea moja kwa moja kambini kuanza maandalizi ya msimu mpya wa 2021/22
Wananchi wanatarajia kuweka kambi nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi taarifa za awali zikibainisha kuwa mabingwa hao wa kihistoria wanaweza kuelekea nchini Morocco
Kocha Nasreddine Nabi atakuwa na takribani wiki tatu za kukiandaa kikosi chake kabla ya kushuka dimbani mwanzoni mwa mwezi Septemba katika hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa
Aidha kabla ya michuano hiyo, ufunguzi wa msimu mpya kwa Yanga utatanguliwa na mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi ambao utapigwa mwanzoni mwa mwezi wa tisa
Ligi Kuu itaanza mwishoni mwa mwezi Septemba ikitanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba utakapigwa Septemba 25