Yanga imeyaaga mashindano ya kombe la Kagame baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutka kwa Express Fc
Wananchi hawakuwa vizuri leo, Express ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi, ushindi ni matokeo waliyostahili
Yanga ilionyesha kandanda safi kwenye dakika 20 za mwisho ambapo walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa shuti la nje ya 18 lililopigwa na Paulo Godfrey 'Boxer'
Kiuhalisia ingekuwa ni miujiza kwa Yanga kufanya vizuri katika michuano hiyo kutokana na aina ya kikosi walichotumia tofauti na wapinzani wao wa kundi A Express na Nyasa Big Bullets waliotumia vikosi vyao vya kwanza
Aidha michuano hii itawasaidia viongozi wa Yanga kuamua hatma ya baadhi ya wachezaji
Express na Nyasa Big Bullets zimetinga fainali, Big Bullets wakiichapa Atlabara mabao 2-0