Huyo kipa mpya wa Yanga ni balaa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Aug 2021
Huyo kipa mpya wa Yanga ni balaa

Ni suala la muda tu mlinda lango Djigui Diarra atatambulishwa kuwa mchezaji wa Yanga akitua kutoka klabu ya Stade Malien ya Mali

Diarra mwenye umri wa miaka 26, alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Mali msimu uliopita, akishinda tuzo hiyo kwa mara ya pili

Akiwa na Stade Malien, Diarra alishinda taji la ligi kuu kwa misimu minne mfululizo kuanzia 2013 mpaka 2017

Akiwa na timu ya Taifa, Diarra alishiriki fainali za Afcon 2016 huku mapema mwaka huu akiongoza timu ya Taifa ya Mali kwa wachezaji wa ndani, yeye akiwa nahodha katika michuano ya CHAN ambayo Mali iliweza kutinga fainali

Kacheza kombe la dunia U-20 akiisaidia Mali kumaliza katika nafasi ya tatu. Mwaka 2015 alitajwa kuwa kipa bora namba 2 kwa ubora barani Afrika

Ni Kocha Nasreddine Nabi aliyependekeza usajili wa mwamba huyu, akiwataka viongozi wa Yanga wamlete Jangwani kwa gharama yoyote

Ni kwa sababu atakuwa na uhakika lango la Yanga litakuwa katika mikono salama chini ya Diarra

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
45m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’