Baada ya uongozi wa Yanga kutangaza kuachana na magolikipa Metacha Mnata na Farouk Shikhalo, ni wazi Ramadhani Kabwili ataendelea kushikilia nafasi yake akiwa mlinda lango namba tatu
Aidha mlinda lango wa Kimataifa wa Mali Djigui Diarra aliyetambulishwa mwishoni mwa wiki iliyopita, anatarajiwa kuwa kipa namba moja
Atasaidiana na Mtanzania Erick Johora aliyesajiliwa kutoka klabu ya Aigle Noir ya nchini Burundi

Johora ameonyesha kiwango bora akiwa na Aigle Noir wakati kwa upande wa Diarra hakuna mwenye mashaka na uwezo wake
Msimu uliopita sare nyingi zilichangiwa na makosa langoni, mabosi wa Yanga wameamua kumaliza changamoto hiyo kwa kuwaleta walinda lango wa viwango vya juu
ADVERTISE HERE