Usajili ambao Yanga wanafanya unalenga kuboresha maeneo yaliyokuwa na changamoto lakini kubwa zaidi ni kusajili wachezaji wenye uzoefu mkubwa ili kuongeza nguvu katika michuano ya ligi ya mabingwa
Mashabiki wa Yanga wana kila sababu ya kufurahia na kupongeza kile kinachofanywa na GSM katika usajili
Shabani Djuma, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Khalid Aucho na Djigui Diarra haya majembe ya kazi kwelikweli
Hapa viongozi wa Yanga na wadhamini GSM wameonyesha dhamira yao katika kujenga timu imara
Usajili umezingatia mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi pamoja na kuwa baadhi ya wachezaji gharama za kuwapata zilikuwa juu
Sawa, taarifa za Tuisila Kisinda kuuzwa zimewaumiza wengi, lakini nafikiri muhimu ni kwa mashabiki kuwa na subira kuona ni nani ataletwa kuchukua nafasi yake
Ni wazi huyo atakayeletwa atakuwa na uwezo sawa au zaidi ya Kisinda kwa kuangalia aina ya usajili wa nyota wa Kimataifa ambao Yanga wanasajili
Jambo moja la uhakika ni kuwa msimu ujao, Yanga itakuwa imara zaidi ya vile ilivyokuwa msimu uliomalizika
Timu itakuwa na wachezaji bora, wenye kiu ya kupata mafanikio kama yalivyo malengo ya klabu



