Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema kutokana na mabadiliko ya kanuni yaliyofanywa, wachezaji wa kigeni watakaosajiliwa na timu nchini watakuwa 12
Karia amesema timu zitaruhusiwa kutumia kwenye kikosi wachezaji 8 tu wa kigeni katika mashindano ya ndani
Karia amesema mabadiliko hayo yamefanyika baada ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kuongeza idadi ya wachezaji kuwa 40 kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona
Aidha Karia amesema walipokea maombi kutoka kwa klabu zinazoshiriki michuano ya CAF
ADVERTISE HERE