Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Injinia Hersi Said amesema wameanza maandalizi yao vyema nchini Morocco kuelekea msimu mpya wa michuano ya ndani na ile ya Kimataifa
Hersi amesema mpaka sasa wanakosekana wachezaji wawili kikosini
Khalid Aucho ataungana nao kesho Alhamisi huku akibainisha kuwa wanatarajia kumtambulisha mchezaji mwingine ambaye ataungana nao pia
Aidha Injinia Hersi amesema jezi wanazotumia wachezaji huko Morocco ni maalum kwa ajili ya pre-season tu, utambulisho wa jezi kwa ajili ya msimu ujao utafanyika kwa kufuata utaratibu ambao wamekuwa wakiutumia katika misimu miwili iliyopita
ADVERTISE HERE