Yanga inaingia katika mchezo wake wa tatu wa Kundi B Kombe la Mapinduzi itakapomenyana na Taifa Jang'ombe Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia Saa 2:15 usiku.
Mchezo huo unakuja siku moja tu baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKU jana, bao la dakika ya 90 la beki Hassan Ramadhani Kessy.
Yanga SC imefikisha alama sita baada ya mechi mbili,iwapo itapata ushindi leo itakuwa imejihakikishia kwenda Nusu Fainali hata kabla ya mechi zake mbili za mwisho dhidi ya Zimamoto FC Januari 7 na Singida United Januari 8.
Mechi ya kwanza leo itakuwa ni kati ya Mlandege na Singida United Saa 8:30, kabla ya URA kumenyana na Azam FC Saa 10:30 jioni.

ADVERTISE HERE