Baada ya kukumbwa na changamoto katika eneo la lango kwa misimu kadhaa, Yanga ililazimika kusafiri nchini Mali kumchukua mlinda lango Diarra Djigui
Yanga walimng'oa Djigui kutoka klabu ya Stade Malien, mabingwa wa ligi kuu ya Mali
Mlinga lango huyu namba moja wa timu ya Taifa ya Mali, alikuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya nchi hiyo katika msimu uliopita. Alikuwa pendekezo la kocha Nasreddine Nabi
Katika muda mfupi aliokuwa na kikosi huko Morocco, Djigui ameonyesha umahiri mkubwa hadi kuwakosha wachezaji wenzake
Ni kipa ambaye amejipambanua hafungiki kirahisi tu anapokuwa langoni

Mshambuliaji Ditram Nchimbi ni miongoni mwa wachezaji waliovutiwa na Djigui akibainisha kuwa msimu huu kazi ipo
Ni baada ya kumshuhudia akiokoa michomo ya hatari katika mechi za mazoezi jana
Mbali na Diarra, kipa mzawa Erick Johola naye ameonyesha ubora wake. Ameonyesha uhodari wa kudaka mashuti makali hasa ya juu