Tukio kubwa la uzinduzi wa Wiki ya Mwananchi linafanyika leo visiwani Zanzibar
Mgeni rasmi wa tukio hilo ni Hemed Suleiman Abdullah, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar
Kuelekea Uzinduzi huo, jana Viongozi wa Yanga walikabidhi magodoro 30 ya chapa GSM kwa hospitali za Mwembeladu na Mnazi Mmoja Zanzibar
Magodoro hayo yalipokelewa na Mhe. Riziki Pembe Juma Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi

Uzinduzi huo utaashiria Wananchi kujitolea kufanya shughuli mbalimbali za kijamii, kutoa misaada na kuchangia damu
Kilele cha Wiki ya Mwananchi ni August 29 uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo kutakuwa na utambulisho wa kikosi cha Yanga kwa ajili ya msimu ujao
Aidha jezi mpya kwa ajili ya msiimu ujao zinatarajiwa kutambulishwa siku chache kabla ya kilele cha wiki ya Wananchi Jumapili ijayo