Baada ya kujifua nchini Morocco kwa wiki moja, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi Jumapili, August 29
Aidha baadhi ya wachezaji wake wanatakiwa kujiunga na timu za Taifa kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said amesema wachezaji nane wameitwa kujiunga na timu za Taifa
Hersi amesema pamoja na kuondoka kwa wachezaji hao, hali ya hewa ya Morocco imekuwa changamoto kwao kwani joto ni kali
Pia kwa kuzingatia Yanga inaanzia nyumbani mchezo wa kwanza wa michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United, wameona ni vyema kurejea nyumbani kukamilisha maandalizi ya mchezo huu hapa hapa
"Tangu tufike hapa trumekuwa na changamoto ya hali ya hewa hapa Marrakech sasa kuna joto kali sana sasa tumeona ni bora timu irudi nyumbani ambako hali yake ya hewa hata kama kutakuwa na joto lakini sio kama la huku"
"Tuna ratiba pia ya mechi ya wiki ya Mwananchi ambayo itafanyika wiki hii mwishoni lakini pia mnajua kwamba tuna mechi ya hatua ya kwanza ya ligi ya mabingwa palepale nyumbani kwahiyo sababu hizi tumeiona ni bora maandalizi yetu yakafanyike palepale katika kumalizia.
"Tulikuwa tuondoke hapa tareje 27 lakini kuondoka kwetu leo kunatufanya sasa kuondoka kwa makundi mawili kundi la kwanza litaondoka leo na kufika nyumbani Tanzania kesho Jumanne mchana na kundi lingine litaondoka siku chache zijazo"
"Kipo ambacho tumekipata katika kambi hii,walimu wamepata muda wa kukaa na wachezaji kwa pamoja lakini pia maandalizi yetu yamekuwa yakifanyika katika eneo ambalo linavifaa vya kutosha ambavyo vinaviwango bora,kwahiyo kambi yetu imekuwa ya mafanikio," alisema Hersi