Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeelekea DR Congo kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Qatar mwaka 2022
Tanzania itacheza na DR Congo siku ya Alhamisi, Septemba 02 katika mchezo utakaopigwa huko Congo
Baada ya mchezo huo Tanzania itarejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo mwingine dhidi ya Madagascar ambao utapigwa Septemba 07 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Tanzania imepangwa kundi J pamoja na nchi za Benin, Madagascar na DR Congo
Timu kinara wa kundi itatinga raundi ya pili ya mchujo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia huko Qatar
ADVERTISE HERE