Kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi Avic Town Kigamboni kuelekea mchezo wa hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United ambao utapigwa Septemba 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ili kuhakikisha kikosi kinakuwa sawa kabla ya mechi hiyo, Yanga inatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki
Yanga haikuwa na muda mrefu wa pre-season huku wakicheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya DTB kabla ya kuikabili Zanaco Fc katika mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi mwishoni mwa wiki iliyopita
Timu inaendelea na maandalizi pamoja na kuwakosa baadhi ya wachezaji walioitwa timu za Taifa
Msimu huu umekuwa na ufinyu wa muda wa maandalizi kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa baada ya ligi kuchelewa kumalizika pamoja na ushiriki wa michuano ya Kagame