Tanzania imepata alama moja muhimu ugenini baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia
Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa TP Mazembe, uliishuhudia Stars ikisawazisha bao baada ya kutanguliwa na DR Congo waliofunga bao lao la kuongoza kupitia kwa Dieudone Mbokani kwenye dakika ya 23
Alikuwa ni Simon Msuva aliyeihakikishia Stars alama moja muhimu baada ya kufunga bao kwa shuti kali akiwa nje ya 18
Ulikuwa ni mchezo ambao vijana wa kocha Kim Poulsen walicheza vizuri hasa eneo la ulinzi

Ni matokeo ambayo yanaweza kuinufaisha Tanzania katika kampeni yake ya kuwania nafasi ya kucheza kombe la Dunia kwa mara ya kwanza
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Madagascar ambao utapigwa Septemba 07 katika uwanja wa Benjamin Mkapa