Aucho uso kwa uso na Diarra kombe la Dunia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Sep 2021
Aucho uso kwa uso na Diarra kombe la Dunia

Jumatatu Septemba 06, Uganda Cranes itachuana na Mali katika mchezo wa kuwania tiketi ya fainali za michuano ya kombe la Dunia

Kiungo Khalid Aucho atakumbana na mlinda lango Djigui Diarra wote wakiwa wametua Yanga katika usajili wa dirisha lililofungwa hivi karibuni

Wakati Diarra aliweza kushiriki kilele cha Wiki ya Mwananchi licha ya kufiwa na baba yake, Aucho hakuweza baada ya kutakiwa mapema na Uganda iliyokuwa ikikabiliwa ya mechi ya kirafiki kabla ya mchezo wao dhidi ya Kenya uliopigwa jana na kumalizika kwa suluhu ya bila ya kufungana

Habari njema zaidi kwa kocha Nasreddine Nabi ni kuwa wachezaji hao wanaweza kutua jijini Dar es salaam Septemba 07 baada ya kumaliza majukumu yao katika mchezo huo

Nyota wengine Feisal Salum , Dickson Job na Bakari Nondo Mwamnyeto ambao wako kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, nao wanaweza kurejea kambini Septemba 07 baada ya mchezo dhidi ya Madagascar ambao utapigwa siku hiyo katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kiraka Yannick Bangala ambaye yuko katika kikosi cha DR Congo yeye anaweza kutua nchini Septemba 08 kwani DR Congo watakuwa ugenini dhidi ya Benin katika mchezo utakaopigwa Septemba 06

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’