Nabi kumbadilishia majukumu Kibwana Shomari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Sep 2021
Nabi kumbadilishia majukumu Kibwana Shomari

Baada ya usajili wa Shabani Djuma ambaye amechukua majukumu ya safu ya ulinzi wa kulia, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi bado anaonekana kumuhitaji Kibwana Shomari katika kikosi chake cha kwanza na huenda akambadilishia majukumu

Katika mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi uliopigwa wiki iliyopita dhidi ya Zanaco Fc, Kibwana alitumika kama mlinzi wa kushoto, akicheza nafasi hiyo kwa dakika zote 90

Licha ya usajili wa David Bryson ambaye ameungana kwenye safu ya ulinzi upande wa kushoto na Adeyum Saleh na Yassin Mustafa, bado Nabi alipendelea kuanza na Kibwana

Juzi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers, kwa mara nyingine Kibwana alianza katika safu ya ulinzi upande wa kushoto huku Djuma akikaa upande wa kulia

Baadae Nabi alimhamishia Kibwana eneo la kiungo mkabaji kuchukua nafasi ya Zawadi Mauya aliyekuwa ameumia huku Adeyum akiingia kucheza kushoto

Bado Bryson hawaja fit kwa asilimia 100 kwani nae alikuwa majeruhi kama ilivyo kwa Yassin ambaye alikosa karibu mechi zote za duru ya pili msimu uliopita kutokana na majeraha

Kibwana ndiye mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi kwenye kikosi cha Yanga msimu uliopita

Kiwango chake kimeimarika sana, lakini bado sio rahisi kwake kumuweka nje Djuma katika safu ulinzi upande wa kulia

Kwa kuwa Nabi bado anamuhitaji kuanza kwenye kikosi chake, analazimika kumbadilishia majukumu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’