Yanga iko mawindoni kule Avic Town Kigamboni kujiandaa na mechi ya hatua ya awali ligi ya mabingwa wakianzia nyumbani dhidi ya Rivers United ya Nigeria
Mechi ya kwanza itapigwa Septemba 12 pale uwanja wa Benjamin Mkapa na marudiano kupigwa wiki moja baadae Nigeria
Kwa kuanzia, Yanga imelenga kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo. Mabingwa hao wa kihistoria wana takribani dakika 180 kulifanikisha hilo
Kama watavuka hatua ya awali, raundi ya kwanza watacheza na mshindi wa mchezo kati ya Fasil Ketema ya Ethiopia dhidi ya Al Hilal ya Sudan
Mara ya mwisho kwa Yanga kucheza makundi ligi ya mabingwa ni mwaka 1998 ambapo Yanga ilikuwa miongoni mwa timu nane zilizoingia robo fainali wakati huo hatua hiyo ikichezwa kwa mtindo makundi
Msimu wa 2015/16 na 2017/18 Yanga iliweza kutinga makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anaendelea kuwaandaa vijana wake kuhakikisha wanaanza na ushindi Septemba 12