Hii Yanga itakaa sawa, tusubiri

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2021
Hii Yanga itakaa sawa, tusubiri

Hii Yanga inawezakuwa na wakati mgumu kwenye klabu Bingwa Afrika kwa kukosa maandalizi mazuri lakini wakawa moto wa kuotea mbali ligi kuu Tanzania bara na michuano mingine ijayo

Kinachoonekana kwa haraka ni Mwalimu Nasredine Nabi kukosa muda wa kutosha kuiandaa timu kwa michuano hii ya kimataifa

Mchezo wa jana dhidi ya Rivers United dhahiri ulikuwa unaakisi 'struggle' ya Mwalimu kutafuta 'playing partnership' ya wachezaji kwenye 'patterns' zote za kujilinda na kushambulia.

Kama angekuwa na muda wa kutosha wa kukaa na timu ni dhahiri hilo lisingemsumbua.

Kinachotakiwa Uongozi, wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga SC kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote klabu bingwa ili iwape kura ya turufu kujipanga vyema kwa ligi ya ndani ambayo itawasaidia zaidi katika ile mipango yao ya KUUNDA TIMU YA USHINDANI miaka mitano ijayo.

Mapema sana kuanza kulaumiana na kukilaani kikosi cha sasa licha ya uwepo wa Wachezaji wachache ambao ni averaged, kwa sehemu kubwa wana wachezaji wazuri ambao wakiwa blended vyema na hao averaged lastly mtapata mseto mzuri kushindania Ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara , ASFC, Mapinduzi, Kagame na mashindano mengine ambayo si rasmi.

Matatizo wanayopitia Yanga SC kwa sasa si mageni kwa timu ambayo ipo kwenye kujijenga upya kutafuta ubora au kurudia ubora wake .

Klabu inapofanya usajili mkubwa huku ikiacha wachezaji wengi; technically itakumbana na Changamoto za ukamilishaji usajili kwa wakati , kupata wachezaji ambao wanaweza wasiwe bora au kushindwa kuendana na mfumo mwanzoni, pia huathiri benchi la ufundi kwakuwa pia nalo huwa jipya au kama la zamani hupata changamoto ya kukisuka kikosi upya

Kwa hisani ya Samuel Samuel

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’