Moja ya changamoto zilizoikumba Yanga msimu uliopita ambazo kwa kiasi kikubwa zilichangia timu kushindwa kufikia malengo yake ni Mabadiliko ya mara kwa mara ya benchi la ufundi
Msimu uliopita Yanga ilibadili makocha mara nne, msimu huu uongozi wa Yanga umesisitiza hautarudia makosa hayo
Kuna taarifa zimeripotiwa katika baadhi ya magazeti ya leo zinazodai kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amepewa michezo miwili dhidi ya Rivers United na Simba
Na kama hatapata ushindi katika michezo hiyo, mkataba wake na Yanga utasitishwa
Jambo hilo halina ukweli wowote, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Dominic Albinus 'Baba Paroko' amesema taarifa hizo zipuuzwe kwani zinalengo la kuwavuruga Wanayanga
Amesema Yanga ina mpango wa muda mrefu na Kocha Nabi hivyo hawafikirii kuachana nae sasa