Athumani Chama aaga dunia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
8 Jan 2018
Athumani Chama aaga dunia
Beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Athumani Juma ‘Chama’ aliyeweika klabu za Pamba FC ya Mwanza na Yanga ya Dar es Salaam amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Kiharusi.

Chama ni jina la utani ambalo marehemu Athumani Juma alipewa kutokana na beki wa zamani wa kimataifa wa Zambia, Dick Chama ambaye naye ni marehemu aliyecheza kwa mafanikio timu ya taifa ya kwao kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia 1967 hadi 1976 na klabu za Mufulira Wanderers, Green Buffaloes na Bancroft Blades.

Athumani alipewa jina hilo baada ya kujiunga na Yanga SC mwaka 1981 akitokea Pamba ya Mwanza na mashabiki wa timu hiyo ya Jangwani walimbatiza Juma jina hilo baada ya beki wao mwingine, Rashid Idd aliyekuwa akiitwa Chama pia kuhamia Pan Africans baada ya kudumu Jangwani tangu 1979.

Na umaarufu wake zaidi Jangwani ukaja kutokana na alivyoweza kumdhibiti mshambuliaji hatari wa mahasimu enzi hizo, Simba SC, Zamoyoni Mogela ‘Golden Boy’.

Kisoka, Chama aliibukia Pamba FC ya Mwanza alikozaliwa na kukulia kabla ya kujiunga na Yanga SC na aliocheza nao wakati huo ni akina Joseph Fungo, Yussuf Ismail Bana, Ahmed Amasha ‘Mathematician’, Isihaka Hassan Chukwu, Juma Mukambi ‘Jenerali’, Hussein Iddi, Charles Boniface Mkwasa, Abeid Mziba ‘JJ Masiga’, Elisha John, Ali Mchumila, Makumbi Juma ‘Homa ya jiji’, Omar Hussein ‘Keegan’, Juma Kampala na wengineo.

Chama pia alikuwa akijulikana kwa jina lingine la utani, Jogoo ambalo alipewa mwaka 1981 kwenye michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya kutokana na mchezaji mmoja wa Harambee Stars, Sammy Onyango ‘Jogoo’.

Chama alistaafu soka mwaka 1990 na kujikita kwenye biashara zake ndogo ndogo kabla ya kuanza kusumbuliwa na maradhi mwaka 2014 na kujikuta anashindwa kufanya shughuli yake hadi umauti wake.

Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Chama. Amin.

Kwa hisani ya Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE →