Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutokuwa wanyonge kwani wana timu nzuri
Bumbuli amesema walichokutana nacho Nigeria ni funzo kwao katika umuhimu wa kutumia vyema uwanja wa nyumbani
"Wenzetu wametufanyia mambo mengi kututoa mchezoni. Walikuja na mkakati wa kuwazuia wachezaji wetu muhimu wasicheze kwa kisingizio cha covid, wametufanyia mambo mengi ya nje ya uwanja"
"Tunawashukuru wachezaji wetu, wamepambana, tumerejea nyumbani kujipanga kwa ajili ya michuano ya ndani. Mchezo unaofuata ni Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, tunajipanga kuweza kupata ushindi"
"Muhimu kwa mashabiki wetu hawapaswi kuwa wanyonge, tuna timu nzuri na tunajipanga kuhakikisha tunarejesha furaha yao," alisema Bumbuli
Yanga imeondoshwa michunao ya ligi ya mabingwa kwa kupoteza mechi zote mbili dhidi ya Rivers United kwa kufungwa bao 1-0 nyumbani na ugenini
Katika mchezo wa nyumbani Yanga ilikuwa na nafasi ya kushinda kama ingetumia vyema nafasi nyingi walizotengeneza
Kocha Nasreddine Nabi ameeleza changamoto kubwa iliyokabili kikosi chake ni kukosekana kwa muda wa kutosha wa maandalizi huku akiwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu ambao ITC zao zilichelewa