Kiungo Khalid Aucho anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji watakaokuwa katika kikosi cha Yanga kesho kuikabili Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Huu unaweza kuwa mchezo wake wa kwanza kuitumikia Yanga, ikiwa pia ni dabi dhidi ya Simba
Aucho hakutumika kwenye mechi za ligi ya mabingwa kwa kuwa ITC yake ilichelewa kama iliyokuwa kwa Djuma Shabani na Fiston Mayele
Kwa zaidi ya wiki mbili Aucho amefanya mazoezi na wachezaji wenzake kule Avic Town, mwamba yuko tayari
Usajili wake pia unamfanya kuwa mchezaji ambaye anasubiriwa sana na mashabiki kuonekana uwanjani
Aliletwa nchini kwa ajili ya kusajiliwa na Simba lakini GSM 'wakapindua meza' na kufanikiwa kumvuta Yanga
ADVERTISE HERE