Pacha ya Bangala na Aucho ndio tiba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Oct 2021
Pacha ya Bangala na Aucho ndio tiba

Ukiacha mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, katika michezo miwili iliyofuata, Yanga ilikuwa na sura mbili tofauti hasa katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Katika mchezo huo ambao ulipigwa uwanja wa Kaitaba na Yanga kushinda bao 1-0, Wananchi walikuwa bora sana kwenye kipindi cha kwanza lakini wakapunguza makali katika kipindi cha pili hasa baada ya kufanyika mabadiliko ya baadhi ya wachezaji

Hali kama hiyo ilijirudia katika mchezo dhidi ya Geita Gold, hasa katika dakika 30 za mwisho

Lakini haikuwa hivyo katika mchezo dhidi ya Simba, kwani Wananchi walikuwa bora zaidi kwenye kipindi cha pili kuliko walivyocheza kipindi cha kwanza

Katika mchezo dhidi ya Simba eneo la kiungo Yannick Bangala na Khalid Aucho walishirikiana vyema na Feisal Salum 'Fei Toto'

Bangala akarejeshwa kwenye safu ya ulinzi katika michezo dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold baada ya Bakari Nondo Mwamnyeto kupata majeraha ya kidole

Kwa kiasi kikubwa, kukosekana kwa Bangala katika eneo la kiungo ndio kunapelekea Yanga kupungua makali hasa Farid Mussa anapotoka katika kipindi cha pili

Farid amekuwa akitumika kama kiungo mchezeshaji sambamba na Aucho lakini bado hajawa na utimamu wa kucheza dakika zote hivyo mara nyingi katika kipindi cha pili huchoka

Zawadi Mauya ambaye ametumika kama mbadala wake, bado hajaweza kurejea katika makali aliyokuwa nayo msimu uliopita

Mwamnyeto atakapokuwa timamu na Bangala kurudishwa katika eneo la kiungo, bila shaka Yanga itacheza dakika 90 ikiwa na nguvu ileile kama walivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Simba

Bangala ni mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Yanga, ana mapafu ya mbwa!

Lakini pia Mukoko Tonombe amemaliza adhabu ya kukosa mechi tatu, ataongeza nguvu katika eneo la kiungo na hivyo kuipa Yanga uwiano mzuri kwa muda wote wa mchezo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’