Baada ya Benki ya NBC kusaini mkataba wa miaka mitatu ya Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania bara, Bodi ya Ligi imetambulisha nembo mpya ya ligi hiyo
Yanga imekuwa na utamaduni wake linapokuja suala la uchaguzi wa rangi katika jezi zake
Haijawahi kutokea Yanga ikaweka rangi yoyote nyekundu katika jezi yake
Kwa mujubu wa kanuni za uendeshaji wa Ligi, nembo ya NBC (yenye Twiga mwekundu) inapaswa kubandikwa katika upande wa kulia wa mkono wa jezi
Wakati ule wa Vodacom, waliridhia kutoa logo maamum kwa ajili ya klabu ya Yanga (njano, nyeusi)
Bila shaka NBC nao wanaweza utamaduni huo wa Yanga kwa kutoa logo ya ziada ambayo haitakuwa na rangi nyekundu
Huu ni utamaduni wa Wananchi na umeheshimiwa kwa miaka yote na wadhamini waliotangulia!
ADVERTISE HERE