Ijumaa ya tarehe 24 mwezi Juni mwaka 1994 ndani ya mji wa Mbuji-Mayi nchini DR Congo alizaliwa Fiston Kalala Mayele akiwa na uzito wa kilogramu 3.5
Akiwa na miaka saba tu alianza kucheza soka katika shule ya mission ya wakatoliki ndani ya mji wa Mbuji-Mayi
Padre Jean Baques anatanabaisha Fiston alipenda sana kucheza kama kipa ila kutokana na nguvu na uwezo wa kukimbia walianza kumzoesha kucheza ndani nafasi ya kiungo.
Mwaka 2008 familia yake ilihama kutoka mji wa Mbuji-Mayi uliopo ndani ya jimbo la Kasai na kuhamia Kinshasa akiwa tayari ameanza kukomaa kisoka akiwa timu za vijana kama atttacking midfielder
Alipotimiza miaka 18 tu, Les Dauphins Noirs (The Black Dolphins) kama wanavyojulikana kwa jina lao la utani AS Vita klabu waliingia nae mkataba wa miaka mitatu akiwa sehemu ya recruitment ya vijana wa Kinshasa kujiunga na papa mweusi.
"AS Vita ni kama nyumbani kwangu na daima watabaki moyoni mwangu. Urafiki wao na Yanga SC ndio umenifanya niwepo hapa. Mashabiki wetu wengi wa AS Vita wanavaa jezi za Yanga" alizungumza Fiston
Msimu uliopita aliweza kumaliza nafasi ya pili ya ufungaji bora ligi kuu ya DR Congo akitanguliwa na Jean Baleke mshambuliaji wa TP Mazembe. Mayele alifunga goli 13 na Baleke goli 14
Kwa hisani ya Samuel Samuel