Match Day : KMC vs Yanga, Majimaji Stadium

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Oct 2021
Match Day : KMC vs Yanga, Majimaji Stadium

Wananchi wako Songea ambapo jioni ya leo watashuka katika uwanja wa Majimaji kuwakabili watoza ushuru wa Kinondoni, KMC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Ni mchezo muhimu kwa Yanga kuendeleza wimbi la ushindi katika kampeni ya kusaka ubingwa msimu huu

Hata hivyo wanakutana na KMC, moja ya timu zenye kawaida ya kuwapa wakati mgumu katika mechi baina ya timu hizo

KMC ambao ni wenyeji wa mchezo huo walichagua kuupeleka Songea lakini ni wazi wao watakuwa wageni kwani ni Yanga inayotarajia kuwa na mashabiki wengi uwanjani

Tangu Yanga ilipowasili Songea juzi, shamra shamra za Wananchi zimeshamiri kila kona

Idadi kubwa ya mashabiki walijitokeza jana wakati Yanga ikikamilisha maandalizi ya mwisho katika dimba la Majimaji

Hivyo ni mchezo ambao Yanga itakuwa na sapoti kubwa ya mashabiki wake, na hakika wanahitaji kuwapa furaha mashabiki wao ambao wameonyesha upendo mkubwa kwa timu yao

Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 10 jioni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’