Yanga imenufaika na michuano ya kombe la Mapinduzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jan 2018
Yanga imenufaika na michuano ya kombe la Mapinduzi
Pamoja na kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi, Yanga inajivunia kiwango kizuri kilichoonyeshwa na wachezaji wake vijana.

Michuano hiyo imeweza kubainisha hazina kubwa ya wachezaji walio katika kikosi cha Yanga.

Kupitia mashindano hayo wengi tumetambua kumbe Yanga ina wachezaji wengi wanaoweza kufanya vizuri zaidi pengine kuliko wale tuliowazoea kuwaona katika kikosi cha kwanza

Aidha michuano hiyo imewaweka katika wakati mgumu wale wachezaji 'maproo' ambao msimu huu imekuwa bahati mbaya wanalipwa 'mshahara' bila kufanya kazi kutokana na majeruhi mfululizo yanayowaandama.

Tumeshuhudia kuibuka kwa wachezaji kama Said Juma Makapu ambaye hapo awali alikuwa akitumika 'kwa dharura' lakini huenda sasa akawa amejihakikishia namba.

Jana katika mchezo dhidi ya URA Makapu aliibuka nyota wa mchezo wakati juzi pia aliifungia Yanga bao la kusawazisha kwenye mchezo dhidi ya Singida United.

Kocha wa Singida United Hans van Pluijm ambaye ndiye aliyewasajili pamoja na Pato Ngonyani wakati huo akiwa Yanga amesema anawaona vijana hao sasa wameiva.

Bado kuna vijana wengine kama Makka Edward, Said Mussa, Juma Mahadhi, Yohana Nkomola na Ramadhani Kabwili ambao wanahitaji kupewa muda zaidi wa kucheza ili waongeze kujiamini.

Yanga imenufaika zaidi na michuano hiyo na bila shaka kama wachezaji wataendeleza moto waliokuwa nao kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi katika ligi, hakuna shaka ubingwa unaweza kurejea Jangwani kwa msimu wa nne.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’