Nabi aja na mkakati wa kibingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Oct 2021
Nabi aja na mkakati wa kibingwa

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameanzisha utaratibu kwa kikosi chake kupata mechi nyingi za kirafiki ili kuhakikisha wachezaji wote wanaendelea kubaki katika ushindani

Mechi hizo ambazo zitacheza kila baada ya mchezo wa mashindano, zitalenga kuwapatia nafasi wachezaji ambao hawajumuishwi katika kikosi kinachoanza

Nabi amesema mpango huo utawasaidia wachezaji wote kuwa katika ubora na hivyo kuwafanya wawe na utimamu sawa na wale wanaocheza mara kwa mara

"Tumeona tuwe na hizo mechi za kirafiki angalau moja au ikiwezekana mbili kila baada ya mchezo wa ligi. Mechi hii itakuwa maalumu kwa wale ambao hawakucheza mechi ya ligi au wakacheza kwa dakika chache"

"Tunatakiwa kuwa na timu bora yenye kila mchezaji aliye tayari wakati wowote, lakini kama tutakuwa tunawapa muda wa kucheza wale wanaoanza kisha tukawasahau hawa wengine iko siku itatupa shida," alisema Nabi

Msimu huu Yanga imedhamiria kushinda ubingwa wa ligi kuu, benchi la ufundi linaweka mikakati kuhakikisha wanafanikisha mpango huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’