Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesisitiza kuwa klabu hiyo haitaweka rangi yoyote nyekundu katika jezi zake
Manara amesema ni utamaduni ambao wamekuwa nao kwa miaka mingi hivyo lazima uheshimiwe
"Cola Cola ni kampuni kubwa Duniani kila mmoja anafahamu rangi yao rasmi ni nyekundu. Lakini nenda uwanja wa Boca Junior kule Amerika Kusini, wamelazimika kubadili rangi ya mabango yao kuwa 'black and white' kwendana na utamaduni wa Boca Junior ambao kamwe hawatumii rangi nyekundu (inatumiwa na wapinzani wao River Plate) "
"Lakini pia NBC wana nembo yenye rangi nyingine nje ya rangi yao rasmi. Sisi Yanga haitatokea tukaweka rangi nyekundu kwenye jezi zetu," alisema Manara
Hivi karibuni Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli alitoa ufafanuzi wa Yanga kutovaa nembo ya NBC kwenye mchezo wa kwanza akibainisha walikuwa kwenye mchakato wa kumaliza changamoto iliyojitokeza
Hata huyo alisisitiza kuwa Yanga haitaweka doa jekundu katika jezi zake