Mukoko anaamini nyakati nzuri zimerejea kwake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Nov 2021
Mukoko anaamini nyakati nzuri zimerejea kwake

Juzi baada ya nahodha msaidizi Mukoko Tonombe kuifungia Yanga bao la tatu katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, ni kama alizidiwa na furaha na kujikuta akitokwa na machozi

Mukoko ambaye msimu uliopita alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Yanga huku akiingia kwenye kikosi bora cha TFF, amesema kutokana na mapito aliyokumbana nayo karibuni, alijikuta akifikwa na hali hiyo

Nyota huyo kutoka DR Congo amesema tangu atolewe kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho msimu uliopita, tukio lile lilimvuruga na kuchangia kumuondoa mchezoni

Aidha Mukoko alilazimika kukosa mechi tatu za mwanzo wa msimu na hakuweza kurejea kikosini baada ya viunga Khalid Aucho na Yanick Bangala kuwa katika uwezo wa juu sana

"Nikwambie, nimepita wakati mgumu tangu mchezo niliopewa kadi nyekudu (fainali FA), mambo hayakuwa mazuri katika maisha yangu ya soka"

"Kuna wakati nilijikuta nakata tamaa na kulia nikiwa peke yangu kambini na hata nyumbani. Ndio maana nilipofunga bao nilijikuta nalia kwa furaha ambayo ilichanganyikana na huzuni"

"Nawashukuru mashabiki wa Yanga ambao walikuwa nami katika kipindi chote kigumu. Nawaahidi nitaendelea kuwapa furaha," alisema Mukoko

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’