Kama hakutakuwa na mabadiliko ya Ratiba, mchezo wa kwanza wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga utapigwa Disemba 11 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yaani baada ya mechi mbili, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Simba
Kwa mwenendo walioanza nao Yanga msimu huu, ushindi katika mchezo dhidi ya Simba utawaweka katika mazingira mazuri sana kwenye mbio za ubingwa
Hivyo huo ni mchezo ambao sio kwamba Yanga itakuwa ikihitaji kuendeleza ubabe wake dhidi ya Simba tu, lakini inazihitaji alama tatu kunenepesha mtaji wake wa pointi katika mbio za ubingwa
Jana Simba wametangaza kocha mpya raia wa Hispania ambaye 'wachambuzi' wanaendelea 'kumuuza' huko mitandaoni kuwa amewahi kuwa kocha msaidizi wa Real Madrid
Profesa Nasreddine Nabi na Cedric Kaze wanamsubiri sana Disemba 11 ili wamkaribishe rasmi katika ligi kuu ya NBC!