Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli ameksema uongozi wa timu hiyo unafahamu mkataba wa mshambuliaji Ditram Nchimbi unafikia tamati Disemba 15
Bumbuli amesema bado Nchimbi ni mchezaji halali wa Yanga hadi pale mkataba wake utakapomalizika lakini kwa kuwa mkataba uko chini ya mwezi mmoja anaruhusiwa kuzungumza na timu yoyote
Bumbuli amebainisha kuwa Nchimbi atarejea kikosini baada ya kumaliza changamoto zinazomkabili akiwa na ruhusa maalum kutoka kwa uongozi
"Ni kweli Ditram Nchimbi yuko ukiongoni mwa mkataba wake, lakini bado ni mchezaji wetu hadi pale mkataba utakapomalizika. Aliomba ruhusa kurejea kwao kushughulikia matatizo ya kifamilia, tunaamini atakapokamilisha atarejea kikosini"
"Bado uongozi hatujapokea mapendekezo ya kocha hivyo wakati huu yuko huru kufanya mazungumzo na timu yoyote, kama kocha atapendekeza aongezwe mkataba basi uongozi utafanya hivyo," alisema Bumbuli
Nchimbi alitua Yanga mwezi Disemba 2019 katika usajili wa dirisha dogo, akiwatumikia Wananchi kwa misimu miwili akifunga mabao matano na kutoa pasi kadhaa za mabao