Match Day : Namungo Fc vs Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Nov 2021
Match Day : Namungo Fc vs Yanga, NBC PL

Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga jioni ya leo watakuwa uwanjani pale Ilulu mkoani Lindi kuikabili Namungo Fc ukiwa ni mwendelezo wa mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC

Ni mchezo wa kwanza baada ya mapumziko ya kalenda ya michuano ya Kimataifa, Wananchi wakidhamiria kuendeleza wimbi la ushindi

Timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu inakutana na Namungo Fc, moja ya timu ngumu hasa inapocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani

Wananchi wako mkoani Lindi tangu juzi ambapo jana walifanya mazoezi yao ya mwisho katika uwanja wa Ilulu ambao utatumika baadae katika mchezo huo

Yanga imekuwa na maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo wakipata nafasi ya kushiriki maadhimisho ya Mwaka mmoja wa Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi visiwani Zanzibar ambako walicheza mechi mbili za kirafiki

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema vijana wake wako tayari kuelekea mchezo huo huku akibainisha kikosi chake leo kitakuwa na mabadiliko kadhaa

Mshambuliaji Yacouba Songne, atakosekana baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti, jeraha ambalo litamuweka nje kwa miezi mitano

Lakini pia kiungo Khalid Aucho alipata marjeraha wakati akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Uganda

Hivyo kikosi cha Nabi kitakuwa na mabadiliko hayo mawili ya lazima

Yanga inahitaji kushinda ili kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’