Mtanange wa ligi kuu ya NBC kati ya Namungo Fc dhidi ya Yanga uliofanyika uwanja wa Ilulu lIndi, umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Yanga walilazimika kusawazisha bao kwenye dakika ya 81 kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Saido Ntibazonkiza baada ya Feisal kuangushwa katika eneo la hatari
Namungo walitangulia kufunga bao kupitia kwa Obrey Chirwa kwenye dakika ya 51
Katika mchezo huo wachezaji wa Yanga walionekana kukabiliwa na changamoto ya uwanja wakishindwa kucheza soka walilozoea
Namungo walitumia zaidi mipira mirefu na walikuwa bora sana katika kuzuia mashambulizi ya Yanga
Kwa ujumla ulikuwa mc hezo mgumu ambao alama moja inaweza kuwa nzuri kwa Yanga siku ya leo
ADVERTISE HERE