Dakika 630 bila kupoteza mchezo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2021
Dakika 630 bila kupoteza mchezo

Jana Yanga imeangusha alama za kwanza msimu huu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Ilulu, Lindi

Licha ya matokeo hayo, Yanga imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 16 baada ya kushuka dimbani mara sita

Kabla ya matokeo hayo, Yanga ilikuwa imecheza dakika 540 bila ya kupoteza mchezo wala sare!

Walianza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii, wakashinda mechi za ligi kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar (1-0), Geita Gold (1-0), KMC (2-0), AzaM Fc (2-0) na Ruvu Shooting (3-1)

Pamoja na sare ya jana, bado waendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo sasa wakifikisha dakika 630

Yanga pia walishinda michezo yote ya kirafiki waliyocheza katika kipindi hicho

Ligi ni 'marathon', mapambano lazima yaendelee ambapo Yanga inarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza

Mchezo huo utapigwa Novemba 30 katika uwanja wa Sokoine, Mbeya

Kila mchezo kwa Yanga msimu huu ni fainali!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’