Kwani VAR Shilingi ngapi?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Dec 2021
Kwani VAR Shilingi ngapi?

Wiki iliyopita kelele za wale ambao Msemaji wa Yanga Haji Manara anawaita 'wachambuzi chupli-chupli' zilikuwa nyingi sana baada ya Yanga kupata mkwaju wa penati katika mchezo dhidi ya Namungo Fc

Jana yametokea maajabu zaidi hapo uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya mwamuzi Martin Saanya kukataa bao la kusawazisha la Geita Gold kwenye mchezo dhidi ya Simba

Bahati mbaya hutawasikia wale 'wachambuzi chupli-chupli' wakilizungumzia hili

Tutaendelea kusema waamuzi hawa wanafanya makosa kwa sababu ni binadamu, hatujui kama kuna mambo mengine gizani

Lakini nadhani ili kupata suluhu ya makosa haya yanayojirudia kila mara, TFF wanapaswa kufikiria uwezekano wa kuleta VAR nchini

Ni aibu kwa uwekezaji mkubwa unaofanywa na Azam Media katika ligi yetu halafu yanatokea matukio ya uonevu wa waziwazi kwa baadhi ya timu hasa ndogo

Udhamin ambao Azam wameweka kwa ligi kuu ya Tanzania Bara ni mara 10 ya udhamini ambao DSTV wameweka kwa ligi kuu ya Zambia

Lakini Zambia tayari wako kwenye mchakato wa kufunga VAR, kwa nini Tanzania tusifikirie hili?

Nadhani kwa sasa VAR ndio suluhisho la hizi changamoto zinazojitokeza kwani waamuzi watakuwa na nafasi ya kupitia maamuzi yao yenye utata na kuchukua hatua sahihi

Hakuna namna matukio haya yatakwisha kwa sababu zipo adhabu zinatolewa kwa waamuzi lakini hakuna mabadiliko

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’