Siri ya Mayele na mafanikio yake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Dec 2021
Siri ya Mayele na mafanikio yake

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amesema anapokuwa uwanjani anajituma na kutumia akili katika kufunga mabao

Nyota huyo raia wa DR Congo amefichua kuwa kufunga mabao ni kazi anayoipenda zaidi na huwa hana furaha anapotoka uwanjani pasipo kufunga

Amesema jina lake linabeba siri kubwa ya mafanikio yake kwenye soka

"Jina langu la Mayele linamanisha akili, huwa nikifanya kazi zangu kwa kufikili zaidi namna ya kuwa bora, huwa sijisikii vizuri nisipofunga"

"Jina hilo lina tafsiri mengi katika maisha yangu, kwa upande wa soka ndio hayo mnayaona, mengine ni mambo yangu binafsi"

"Sitaki niongee mengi, acha niendelee kupambana na kazi zangu, mashabiki wataona wenyewe, ila tafsiri ya jina langu linaendana na uhalisia wa maisha yangu kwenye maeneo mbalimbali," Mayele alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

Akitua Yanga kutoka klabu ya AS Vita, baada ya mechi saba katika ligi kuu ya NBC, Mayele amejipambanua kuwa moja ya washambuliaji hatari msimu huu

Amefunga mabao matatu katika ligi kuu ya NBC pia akifunga bao pekee kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba

Ndiye mshambuliaji anayetengeneza nafasi nyingi zaidi kwenye ligi. Wengi wamemtabiria kuwa miongoni mwa wachezaji wenye nafasi ya kushinda kiatu cha dhahabu msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’