Udhamini wa GSM ni mzuri - Karia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Dec 2021
Udhamini wa GSM ni mzuri - Karia

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ametoa kauli juu ya udhamini wa GSM baada ya wadau wengi wa soka kuzungumza mengi juu ya mkataba huo.

Wiki moja nyuma GSM ilisaini mkataba wa miaka miwili na TFF wenye thamani ya Sh 2.1 Bilioni wakiwa kama wadhamini mwenza kwenye Ligi Kuu Bara.

Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) uliofanyika jana mjini Morogoro sambamba na uchaguzi mkuu wa Bodi hiyo, Karia alisema udhamini wa GSM ni mzuri tofauti na watu nje wanavyouzungumzia.

"Udhamini wao ni mzuri na sio wamiliki wa timu za Namungo, Coastal wala Yanga, kama ni hivyo basi Coastal Union wasingeifunga Yanga msimu uliopita lakini waliifunga,” alisema Karia na kuongeza;

"Nafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya klabu za Tanzania ili zipate udhamini, tunatafuta udhamini wa mabasi katika kampuni mbalimbali ili tu timu zipate usafiri"

Naye Mkurugenzi wa uwekezaji GSM, Injinia Hersi Said alisema:Β 

"Sisi ni watu imara na hatuwezi kuyumbishwa na watu wengine, naahidi tupo katika hatua za mwisho kwenye kukamilisha mchakato huu"

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’