Ndani ya Mwamnyeto kuna beki, kiungo na mshambuliaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Dec 2021
Ndani ya Mwamnyeto kuna beki, kiungo na mshambuliaji

Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto msimu huu amekuwa mchezaji muhimu sana Yanga inapojenga mashambulizi kutokea nyuma

Katika mabao 12 ambayo Yanga imefunga msimu huu, Mwamnyeto amehusika katika mabao matatu

Alitoa pasi muhimu kwa Feisal Salum iliyowezesha kupatikana bao la pili katika mchezo dhidi ya Azam Fc, akafanya hivyo tena katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting akimuwekea pasi mpenyezo Farid Mussa

Akarudia tena wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza ambapo mpira uliozaa bao la pili ilianzia kwake

Msimu uliopita tulimshuhudia Mwamnyeto tofauti, alikuwa akifunga mabao kwani aliamaliza msimu akiwa na mabao matatu

Hawa ndio aina ya Walinzi ambao kocha Nasreddine Nabi anawahitaji katika kikosi chake

Jukumu la beki sio kuzuia tu bali pia kutengeneza mashambulizi na Mwamnyeto amekuwa akitumika zaidi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi 

Yanga hii ya Nabi usijidanganye kama unaweza kudhibiti mchezaji mmoja mmoja kwani kuna wachezaji wengi ambao wanaweza kutengeneza nafasi na hata kufunga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’